Star Tv

Watu wapatao 1,941 wamekufa kutokana na tetemeko lililopiga Haiti siku ya Jumamosi.

Watu wapatao 10,000 wamejeruhiwa na wengine wengi hawafahamiki walipo baada ya tetemeko lenye ukubwa wa 7.2 katika vipimo vya Ritcher.

Shughuli ya uokoaji bado inaendelea baada ya mvua kubwa iliyopiga wiki hii.

Umoja wa Mataifa umesema, watoto wapatao 500,000 wanahangaika kupata malazi, maji safi na chakula.

"Familia nyingi za Haiti ambazo zimepoteza kila kitu kutokana na tetemeko la ardhi , sasa hivi wanakaa eneo la maji kutokana na mafuriko," alisema Bruno Maes, mwakilishi wa shirika la kimataifa linaloshughulika na ufadhili kwa watoto (UNICEF).

Watu elfu kumi wamebaki bila makazi kutokana na tetemeko la ardhi na majengo mengi yakiwa yamebaki na nyufa.

Kusini magharibi mwa Haiti kunaonekana kuwa kumeathirika zaidi na tetemeko haswa katika mji wa Les Cayes.

"Jana Jumanne jioni, nilipata makazi karibu na kanisani lakini nilisikia ardhi ikitetemeka tena ,nilikimbia na kurudi hapa,"- Alisema mkazi mmoja wa mji wa Magalie Cadet alinukuliwa na wakala wa habari wa AFP.

Aidha baadhi ya hospitali zilikuwa zimelemewa na zilikuwa zina uhitaji wa dawa ili kuweza kutibu waliojeruhiwa.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.