Star Tv

Mkosoaji wa utawala wa Kremlin nchini Urusi Alexei Navalny ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa instagram kwamba anazuiliwa katika kambi ya mateso eneo la Vladimir Kaskazini Mashariki mwa mji mkuu, Moscow.

Katika taarifa hiyo Navalny amesema anazuiliwa katika eneo lenye ulinzi mkali la gereza hilo.

Navalny alikuwa hajulikani aliko baada ya timu yake ya mawakili kusema wiki iliyopita kwamba alikuwa amehamishwa kutoka gereza la Kolchugino na kwamba hawakujulishwa alikopelekwa.

Vyombo vya habari vya Urusi vimemnukuu wakili wa Navalny Olga Mikhailova akithibitisha anazuiliwa katika gereza hilo akisema hajafanikiwa kwenda kumtembelea.

Navalny mwenye umri wa miaka 44 alipelekwa gerezani mapema mwaka huu kwa kukiuka masharti ya msamaha wake, uamuzi ambao nchi za Magharibi zimeukosoa zikisema ulichochewa kisiasa.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.