Star Tv

Kampuni ya AstraZeneca imebainisha kuwa kwasasa tayari imeanza kuelemewa katika hatua yake ya kusambaza chanjo hiyo ya kudhibiti COVID-19 barani Ulaya.

Kampuni ya Uingereza na Sweden inayotengeza chanjo ya AstraZeneca ambayo inaaminika kupambana na maambukizi ya Corona, imetangaza kuwa inakabiliwa na uhaba wa chanjo hiyo kupeleka katika nchi za Umoja wa Ulaya.

Kampuni hiyo ya AstraZeneca inasema inasikitika kuwa inashindwa kusambaza chanjo hiyo katika mataifa ya Ulaya kama ilivyotarajiwa, licha ya juhudi za kutengeneza na kusambaza chanjo hiyo.

Awali, kampuni hiyo ilikuwa imeonya kuwa inakabiliwa na uhaba wa chanjo hiyo barani Ulaya kwa sababu ya changamoto inayoshuhudiwa katika mitambo yake ya uzalishaji.

Katika hatua nyingine, maduka, Mikahawa na Shule zitafungwa kuanzia siku ya Jumatatu wiki ijayo, nchini Italia, baada ya nchi hiyo ya bara la Ulaya kuanza kushuhudia ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona.

Waziri Mkuu Mario Draghi amesema serikali imelazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na mlipuko mpya unaoshuhudiwa nchini humo.

Aidha, kipindi cha pasaka kati ya tarehe 3 hadi 5 mwezi Aprili, nchi hiyo itafungwa kabisa, kwakuwa ni mojawapo ya nchi ambayo imeripoti vifo zaidi ya 100,000 na kuwa taifa la pili kwa vifo barani Ulaya, baada ya Uingereza.

Italia ilikuwa nchi ya kwanza duniani kuweka katazo la watu kutoka nje baada ya kuripotiwa vifo vingi vinavyotokana na maambukizi ya virusi vya corona ambavyo vimewaathiri Mamilioni ya watu Ulimwenguni.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.