Star Tv

Rais wa Marekani Joe Biden amesema ifikapo Mei Mosi mwaka huu, kila Mmarekani mwenye miaka 18 ataweza kupata chanjo ya COVID-19.

Biden amesema hayo katika hotuba yake kwa taifa hilo usiku wa kuamkia Ijumaa.

Rais Biden ameyasema hayo katika hotuba ambayo imetolewa sambamba na maadhimisho ya mwaka mmoja tangu shirika la afya ulimwenguni - WHO kuvitangaza virusi vya corona kuwa janga ya kidunia

''Kwanza usiku wa leo natangaza kuwa nitayaelekeza majimbo yote, makundi ya kikabila na maeneo yaliyo chini ya himaya ya Marekani, kuhakikisha kuwa watu wote wenye umri wa miaka 18 na zaidi, watakuwa na haki ya kupata chanjo kabla ya Mei mosi''- Amesema Biden.

Kiongozi huyo ameanisha pia hatua nyingine za kupamba na ugonjwa huo ambao tayari umeangamiza maisha ya Wamarekani zaidi ya 530,000.

Rais huyo amesema mnamo mwaka mmoja uliopita, Wamarekani wameungana katika maumivu na majonzi, na kuongeza kuwa vile vile wanaunganishwa na matumaini mema ya siku za usoni.

Ametabiri juu ya uwezekano wa Wamarekani kuweza kujumuika tena katika makundi madogo madogo wakati wa sherehe za uhuru wa nchi yao zinazofanyika tarehe nne Julai; lakini ikiwa kabla ya hapo wataendelea kuheshimu maelekezo ya wataalamu wa afya.

Biden ameitoa hotuba yake hiyo baada ya kusaini sheria ya mpango wa afueni wenye thamani ya dola trilioni 1.9, ambao amesema utasaidia kuvishinda virusi vya corona, kuufufua uchumi na kuwapa Wamarekani wenye mahitaji msaada wa moja kwa moja wa kifedha.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.