Marekani imebadili uamuzi wa kulegeza kwa muda, vikwazo dhidi ya Bilionea wa Israel Dan Gertler, anayekabiliwa na tuhuma za ufisadi unaohusisaha biashara ya madini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Hatua hiyo ya hivi punde inabatilisha uamuzi uliotolewa siku za mwisho za utawala wa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.
Mwaka 2017 na 2018, hazina ya Marekani iliweka vikwazo dhidi ya Bw. Gertler ambayo ilimzuia kufanya biashara na raia wa nchi hiyo na taasisi zake, hatua ambayo ilimzuia kupata huduma za benki za kimataifa.
Ilimtuhumu kwa ufisadi na ukiukaji wa maadili katika sekta ya madini na kutumia ushirikiano wake na rais wa zamani wa DR Congo, Joseph Kabila kupata mikataba ya kibiashara.
Hata hivyo, Bw. Gertler amekana kufanya makosa yoyote.
Utawala wa Trump ulikuwa umemuondolea vikwazo Bw. Gertler kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi Januari 31, mwaka 2022, kuendelea kufanya biashara na kampuni za Marekani.
Chanzo:BBC Swahili