Dunia inaadhimisha leo siku ya kimataifa ya Wanawake, kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ''Wanawake katika uongozi: Kufikia mustakabali ulio sawa katika dunia yenye janga la COVID-19.''
Katika taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres sambamba na maadhimisho haya, kiongozi huyo amehimiza kuwashirikisha kikamilifu wanawake katika sekta zote za maendeleo.
Aidha,Mbali na kutoa msisitizo huo, Katibu Mkuu amesema anasikitishwa kuona kuwa hadi sasa uwakilishi wa wanawake katika nafasi za kuchukua maamuzi bado ni wa kiwango cha chini.
Ametoa mfano kuwa wanawake ni viongozi wa serikali za nchi 22 tu duniani, ikiwa asilimia 24.9 tu ya viongozi wote katika wadhifa wa ngazi hiyo.
Aidha, Kaulimbiu ya mwaka huu inahimiza nafasi sawa kwa kizazi cha sasa, ili kufanikisha usawa wa kijinsia mnamo miaka ijayo.