Star Tv

Wanamgambo wa kundi la Al Shabab nchini Somalia wamekiri kuwa wao ndio wametekeleza shambulio kubwa katika hoteli maarufu huko Mogadishu, inayotembelewa na maafisa wa serikali, na kuwaua raia kumi na afisa mmoja wa polisi, kulingana na ripoti rasmi iliyotolewa usiku wa kuamkia leo Jumatatu.

Washambuliaji hao walilipua bomu lililotegwa ndani ya gari nje ya hoteli hiyo Jumamosi usiku kabla ya kuivamia na kuwateka nyara watu.

Ilichukua saa nne ili vikosi vya usalama viweze kupata udhibiti wa Elite Hotel, hoteli maarufu iliyojengwa kwenye pwani ya Lido inayotembelewa mara kwa mara na viongozi wa Kisomali.

Shambulio hilo lilitekelezwa na wanamgambo watano mapema jioni, Ismael Mukhtaar Omar, msemaji wa Wizara ya Habari ameliambia shirika la habari la AFP kuwa "Watu kumi wameuawa, pamoja na washambuliaji watano na afisa mmoja wa polisi".

Wakati huohuo watu 250, raia lakini pia wanasiasa na wabunge, waliokuwa katika hoteli hiyo waliondolewa. Abdirasak Abdi, afisa mwandamizi katika wizara ya habari ni miongoni mwa watu waliouawa katika shambulio hilo.

Katika vifo vilivyoripotiwa Abdirasak Abdi ambaye alikuwa Afisa Mwandamizi katika Wizara ya Habari ni miongoni mwa watu waliouawa kwenye shambulio hilo.

Hata hivyo Vikosi maalumu vya Somalia vinasema vimemaliza uvamizi huo.

Vikosi vya usalama viliizingira hoteli hiyo na kukabiliana kwa risasi na washambuliaji waliokuwa na silaha ndani ya hoteli. Saa nne baadae, msemaji wa serikali Ismael Mukhtaar Omar alituma ujumbe kwenye ukurasa wa Tweeter akisema kuwa uvamizi huo umekwisha na wavamizi wote wameuawa.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.