Star Tv

Leo Jumatatu Rais wa Cameroon Paul Biya, anaadhimisha miaka 35 uongozini na kumfanya kuwa Rais aliyehudumu kwa miaka mingi zaidi barani Afrika.

Bwana Biya aliingia kwa mara ya kwanza uongozini mwaka 1982, wakati taifa hilo lililikuwa chini ya mfumo wa utawala wa chama kimoja.

Hata hivyo, licha ya taifa hilo kwa sasa liko katika mfumo wa uongozi wa vyama vingi vya kisiasa, amefaulu kusalia mamlakani kwa miaka hii yote.

Mnamo mwaka 2011, baada ya katiba ya taifa hilo kuamua mabadiliko yenye utata ya kumruhusu kuwania kiti cha Urais tena, alifaulu kushinda tena uchaguzi mkuu kwa asilimia 78 ya kura zote zilizopigwa na kusalia mamlakani kwa miaka mingine saba.

Ushindi huo mkubwa, uliwafanya wakosoaji wake wengi kuhoji na kushuku uhalali wa uchaguzi huo.

Bwana Biya ni sehemu ya kundi la viongozi kadhaa Afrika, ambao wametawala mataifa yao kwa zaidi ya miaka 30: Wao ni pamoja na Robert Mugabe wa Zimbabwe na Teodoro Obiang Nguema Mbasogo wa taifa dogo la Equatorial Guinea, ambao wangali wakishikilia mamlaka.

Bwana Biya mwenye umri wa miaka 84, na ambaye wakosoaji wake wanamtuhumu kwa kuongoza taifa kiimla, anatarajiwa kuwania tena kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu mwaka ujao wa 2018.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.