Star Tv

Serikali ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo imetangaza kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola katika maeneo mapya.Hali ya wasiwasi imetanda katika maeneo mengi ya mashariki mwa Congo,baada y'a wizara ya afya kutangaza kugundulika kwa ugonjwa wa Ebola katika maeneo ya Beni mashariki mwa nchi hio. Serekali ya Kongo imetangaza hayo wiki moja tu baada ya shirika la afya duniani WHO na mamlaka za DRC kutangaza mafanikio na mwisho wa janga hilo la Ebola katika jimbo la Ecuador.

Wizara ya afya ya Nchini Kongo imetoa taarifa kwa shirika la afya duniani WHO kuwa, vipimo 4 kati ya 6, vimekutwa na virusi vya ugonjwa huko Kinshasa, bado vipimo vingine vinaendelea. Mkurugenzi wa WHO Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kuwa, ebola ni tishio kubwa nchini DRC, lakini uwazi na ukweli wa serikali ya Kongo katika kutoa taarifa za ugonjwa huo, ndio njia ya kwanza ya kuweza kufanikisha mapambano ya kumaliza Ebola DRC.

Mkurugenzi wa WHO kwa upande wa Afrika amesema ni rahisi kuanza mara moja jitihada za kuzuia Ebola kwasababu wametoka kupambana na tatizo hilo hilo, hivyo vifaa na wafanyakazi wako tayari. Maambukizi makubwa yameonekana katika eneo la Mangina ambapo ni kilomita 30 tu kutoka mji wa Beni. ''tatizo hili limetokea katika mazingira tofauti na yale tuliokua tukifanya kazi mara ya kwanza katika eneo la kaskazini mashariki'' amesema Dr Peter Salam msaidizi wa Mkurgenzi wa WHO.

Kivu Kaskazini ina watu zaidi ya milioni Moja walitoka maeneo mbalimbali hasa Uganda na Rwanda ambapo wanatumia Mpaka mmoja katika shughuli za kibiashara. WHO inaendelea kufanya kazi na nchi jirani kuhakikisha kuwa mamlaka za Afya zinapata taarifa na kujiandaa.

Kwa hisani ya BBC

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.