Star Tv

Kumekuwa na maandamano katika miji mbalimbali nchini Sudan Kusini mara baada ya gharama ya mkate kuongezeka mara mbili zaidi.

Hatua hiyo ya maandamano imekuja baada ya serikali ya nchi hiyo kufanya maamuzi ya kuondoa ruzuku ya vyakula na kusababisha gharama ya mkate kuwa kubwa mara dufu.

Huko magharibi mwa Darfur, mwanafunzi mmoja aliyekuwa katika maandamano aliuwawa na wengine sita kujeruhiwa mara baada ya maandamano hayo kugeuka kuwa ya fujo.

Katika mji mkuu wa Khartoum, polisi walitumia mabomu ya machozi kusambaratisha watu ambao walikuwa wamefunga barabara na kuchoma matairi.

Naibu waziri wa mambo ya ndani alikanusha kuwa maandamano hayo hayakutoea kutokana na ongezeko la bei na kuahidi kuwa atawashughulikia wale wote waliokuwa wanafanya maandamano yenye fujo.

Serikali ya Sudan pia imezuia magazeti yote yaliyokosoa ongezeko la bei kutouzwa. Maamuzi ya kuongeza bei ya mkate kwa serikali ya Sudan ni sehemu ya kufuata matakwa ya IMF ili kukuza uchumi wa nchi hiyo.

Kwa hisani ya BBC.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.