Star Tv

Cyril Ramaphosa amechaguliwa kuwa kiongozi mpya wa chama tawala cha ANC nchini Afrika Kusini .

Ramposa ambaye alikuwa makamu wa rais wa chama hicho aliweza kumshinda mpinzani wake Nkosazana Dlamini-Zuma, ambaye ni waziri wa zamani na alikuwa mke wa rais Zuma kwa kura 2440 kwa 2161.

Kwa sasa Ramaphosa ameonekana kuwepo kwenye nafasi kubwa ya kuwa rais katika uchaguzi wa mwaka 2019.

Hata hivyo Cyril Ramposa amekuwa kiongozi wakati ambao Afrika kusini inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinafanya mambo hayendi sawa katika taifa hilo .

Cyril Ramposa alizaliwa tarehe 17 mwezi novemba mwaka 1952 mjini Soweto, ndio mwanasiasa tajiri zaidi Afrika Kusini ,utajiri wake unakisiwa kuwa ni dola milioni 450.

Tangu ujana wake Ramposa alikuwa na ndoto ya kuwa mwanasiasa shupavu na hiyo ndio ilimfanya kujiunga na uongozi wa chama cha wafanyakazi .

Na wakati chama cha ANC kilipochukua uongozi wa Afrika kusini mwaka 1994,alitamani sana kuwa naibu wa mwasisi wa Afrika Kusini mpya ,Nelson Mandela lakini pale Mandela alipompuuza na badala yake kumteua Jacob Zuma inasemekana kuwa bwana Ramaphosa alisusia hata sherehe za kuapishwa kwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini vilevile alisusia kuchukua wadhifa wowote wa uongozi katika serikali mpya ya Afrika Kusini .

Jacob Zuma na makamu wake walazimishwa kusalimiana Badala yake bwana Cyril Ramaphosa ambaye alisomea uwakili alihiari kuwa mbunge na mwenyekiti wa bunge la katiba ambalo lilishughulikia kutengeneza katiba ambayo ilisifiwa sana duniani.

Badaye Ramaphosa alishangaza wengi alipojiuzulu kutoka kwenye siasa na kushughulika zaidi katika biashara zake,lakini mwaka 2012 alishawishika tena na kurudi kwenye siasa na kuwa na ilipofika mwaka 2014,alipanda zaidi na kuwa makamu wa rais Zuma.

Na wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kurudi kwake Ramaphosa kwenye chama cha ANC kulirudisha imani ya wananchi wengi licha ya kuwa chama hicho kilikuwa kinakabiliwa na kashfa nyingi za kisiasa.

Kwa hisani ya BBC

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.