Star Tv

Vikosi vya usalama nchini Sudan vimerusha vitoa machozi kwa waandamanaji ambao wanapigania demokrasia katika mji mkuu wa Khartoum.

Walimu waliokuwa wakishiriki katika mojawapo ya maandamano hayo walikamatwa na vikosi vya usalama.

Usiku kucha waandamanaji waliweka vizuizi kwa siku mbili za kwanza za maandamano ili kupinga mapinduzi ya kijeshi ya mwezi uliopita.

Wanataka serikali ya kijeshi kujiuzulu na kuruhusu mpabadiliko ya amani.

Maandamano hayo yanafanyika huku wapatanishi wa Muungano wa mataifa ya Kiarabu {Arab League} wakiwasili mjini Khartoum kwa mazungumzo ili kujaribu kusitisha tatizo hilo.

Waziri mkuu Abdalla Hamdok, bado amewekwa katika kifungo cha nyumbani na anakabiliwa na shinikizo kutoka kwa wanajeshi hao kushirikiana nao, mwandishi wa BBC Andrew Herding amesema kutoka mji huo mkuu.

Mwezi uliopita, kiongozi wa mapinduzi hayo Jenerali Abdel Fattah al – Burhan, alifutilia mbali utawala unaoongozwa na raia, kuwakamata viongozi wa kiraia na kutangaza hali hatari.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.