Kiongozi wa zamani wa Baraza la jeshi nchini Mali Kanali Assimi Goïta amejitangaza kuwa rais wa mpito baada ya kuwavua madaraka rais wa mpito na Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo.
Rais Bah Ndaw na Waziri Mkuu Moctar Ouane waliokuwa katika kambi ya kijeshi usiku wa Jumatatu kwasasa wameachiwa huru kutoka kizuizi cha kijeshi.
viongozi hao walipelekwa katika kambi ya kijeshi usiku wa Jumatatu katika hatua ambaye iliifanya Mali kukabiliwa na mapinduzi ya pili ya kijeshi ndani ya miezi tisa.
Hatua hiyo ilichochewa na mageuzi katika baraza la mawaziri ambapo maafisa wawili wa jeshi waliohusika na mapinduzi ya awali walipoteza kazi zao.
Kanali Goïta alilalamika kwamba rais aliyeondolewa madarakani hakushauriana naye kuhusu baraza jipya la mawaziri.
Aidha, Hali ya taharuki imetanda nchini Mali hivi leo lakini mpaka sasa imeripotiwa kuna utulivu.
ChanzonaBBCSwahili