Wizara ya afya nchini Uganda imetangaza wagonjwa wanne wapya wa virusi vya corona na kufanya idadi ya walioathirika na ugonjwa huo kufikia 79.
Wagonjwa hao wanne ni madereva wa malori kutoka Tanzania waliowasili nchini humo kupitia mpaka wa Mutukula.
Wagonjwa hao ni miongoni mwa sampuli 1,578 zilizochukuliwa kutoka kwa madereva wa malori, ambapo miongoni ni kati ya sampuli za wakazi 411 zilizochukulia ili kufanyiwa vipimo hakuna hata mtu mmoja aliyekutwa na ugonjwa huo isipokuwa madereva hao.
Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya Uganda kuwarudisha nyumbani kwa lazima raia wawili, huku mmoja akiwa ni wa Tanzania na mwingine wa Kenya ambao walikutwa na virusi hivyo.
Aidha, uamuzi huo ulidaiwa kuathiri uhusiano kati ya mataifa hayo wanachama wa Afrika mashariki na hivyo kuhatarisha usafirishaji wa mizigo kati ya nchi hizo.