Wizara ya Afya Uganda imetangaza ongezeko la mgonjwa mmoja wa COVID-19, ambapo mgonjwa huyo mmoja wa Corona aliyetangazwa leo anaongeza idadi ya walioambukizwa ugonjwa huo nchini humo kufikia 56.
Wizara hiyo imesema mgonjwa huyo mpya ni mkimbizi kutokea Burundi mwenye umri wa miaka 46 ambaye aliingia Uganda alitokea Tanzania na tayari amewekwa Karantini anapata uangalizi pamoja na matibabu.
Mpaka kufikia aprili 14, watu 54 waligunduliwa kuwa na maambukizi ya virusi hivyo na kati yao wanne walitolewa taarifa yakuwa wamepona.
Marufuku yakukaa ndani ilitangazwa Machi 31 na rais Museveni ambapo aliwataka watu kutokutoka nje kwa siku 14 ambazo ziliisha Aprili 14.
Aprili 14, 2020 wakati akizungumza na vyombo vya habari Museveni aliongeza muda wa siku 21 kwa ajili ya watu kuendelea kusalia majumbani ili kupambana na virusi vya ugonjwa huo, Hatua hiyo inachukuliwa kama njia ya kupunguza kuenea kwa maambukizi ya Virusi vya Corona.