Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam linawashikilia watu 32 watuhumiwa wa wizi wa shilingi Bilioni 2.82 za benki ya NMB wakiwemo wafanyakazi watano wa kampuni ya ulinzi iliyopewa jukumu la kulinda wakati fedha hizo zikihamishwa kutoka tawi la benki hiyo la Mbezi Beach kwenda NMB House Posta Mpya na kutokomea kusikojulikana na gari iliyobeba fedha hizo.
Hata hivyo Jeshi hilo limekamata gari hiyo na kukuta masanduku matatu yenye shilingi Bil. 1.3 na silaha aina ya short gun pump Action yenye risasi 12 na short gun protector yenye risasi 5 na sare za kampuni hiyo ya ulinzi.
Jeshi hilo limesema limefanya juhudi za kuhakikisha fedha hizo ambazo ni mali za Watanzania zinapatikana, na kusema kuwa watu hao walioshiriki katika wizi wa fedha hizo japokuwa tayari walishanunulia vitu vya thamani kwa njia ya utakatishaji fedha na tayari wameshawakamata.