Star Tv

Shirika la Afya Duniani limesihi watu kutoweka imani zao kwa dawa za mitishamba zinazotengenezwa na wenyeji kwa misingi ya kudai zina uwezo wa  kukabiliana na virusi vya corona.

Hatua hiyo imekuja baada ya marais karibu wanne wa Afrika kusema wanaagiza dawa ya mitishamba iliyosemekana imepatikana Madagascar kuwa ina uwezo wa kutibu virusi vya corona.

Shirika la Afya Duniani limepata taarifa zao na kutoa onyo juu ya dawa hizo wakati ambapo kila mmoja duniani ana hamu ya kupata dawa ya kutibu ugonjwa huo.

Shirika hilo limesema ni muhimu dawa zinazosemekana kuwa na uwezo wa kutibu kufanyiwa majaribio kabla hazijaanza kutumika na kuonya kuwa huenda watu wakaona wamepata tiba na kujihisi kuwa salama na kumbe hazina uwezo wa kutibu.

Viongozi wa Afrika ambao tayari wamezungumzia kwenda kuchukua dawa hiyo ni rais Magufuli, rais wa Jamuhuri ya Congo, Guinea Bissau na Equatorial Guinea.

Dawa hiyo inayohusishwa na mmea wa Kichina unaoitwa Artemisia(pakanga) ambao ni mojawapo ya miti ambayo huchanganywa pamoja na mimea mingine ya Madagascar kama tiba ya ugonjwa wa Malaria.

Aidha, rais wa Madagascar Andry Rajoelina amesema nchi yake itaanza majaribio ya kitabibu ya kinywaji cha mitishamba ambacho anakipigia upatu kuwa kinauwezo wa kuzuia na kutibu corona.

Pia amewataka wananchi wake kupanda kwa wingi mmea ambao unaotomika kutengeneza kinywaji hicho ambacho kimepewa jina la Covid-Organics.

Rais Rajoelina amesema kwa sasa anatafuta kibali cha WHO ili kuwa kinywaji hicho kuwa dawa ya kutibu Corona.

Hata hivyo msimamo wa Shirika la Afya kuhusu kinywaji hicho mpaka sasa haujabadilika na wanaonya watu dhidi ya dawa mbadala kutumika kama kinga ama tiba ya corona.

Mpaka kufikia sasa watu zaidi ya milioni 3.5 duniani kote wamethibitishwa kupata maambukizi ya virusi vya corona, watu zaidi ya laki mbili na hamsini wamefariki dunia huku watu zaidi ya milioni moja wamepona.

Latest News

FELICIEN KABUGA KUSHTAKIWA MAHAKAMA YA UN.
03 Jun 2020 17:11 - Grace Melleor

Mahakama nchini Ufaransa imeagiza Félicien Kabuga ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda kufikishwa [ ... ]

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI KESI YA SPIKA NDUGAI NA MWAMBE.
03 Jun 2020 14:49 - Grace Melleor

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wakili Paul Kaunda dhidi ya Spik [ ... ]

CHADEMA YAFUNGUA MILANGO KWA WANAOTAKA KUGOMBEA URAIS.
03 Jun 2020 14:33 - Grace Melleor

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefungua milango kwa wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea nafasi ya [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.