Star Tv

Mwanamfalme Charles wa Wales mwenye umri wa miaka 71 amekutwa na maambukizi ya virusi vya corona huku taarifa kutoka kwa msemaji wa familia hiyo ya kifalme zikieleza kuwa mwana wa mfalme huyo ameonyesha dalili ndogo za maambukizi ya Corona kwa sasa lakini bado amebakia kuwa katika afya nzuri.

Mkewe Mwanamfalme huyo aitwaye The Duchess of Cornwall, mwenye umri wa miaka 72 pia amefanyiwa vipimo , Na baada ya vipimo hivyo vimeonyesha kuwa hana virusi hivyo.

Makao yao ya Ufalme Clarence House yamesema kuwa Charles na Camilla kwa sasa wamejitenga binafsi katika makazi ya Balmoral, na kuongeza kuwa mwanamfalme amekua akifanyanyia kazi nyumbani kwa kipindi chote cha siku chache zilizopita.

Aidha, vipimo vilichukuliwa na mamlaka ya kitaifa ya huduma za afya nchini Uingereza eneo la Aberdeenshire, ambako walitimiza vigezo vya kupimwa na kutolewa majibu.

Taarifa kutoka kwenye familia hiyo zinaeleza kuwa huenda isiwe rahisi kutambua mwanamfalme aliambukizwa na nani virusi hivyo ikizingatiwa idadi kubwa ya watu ambao aliokutana nao katika kazi zake za umma katika wiki za hivi karibuni.


Msemaji wa mwanamfalme amezungumza na Malkia pamoja na mtoto wake The Dukes of Cambridge na Sussex na imefahamika kuwa wameipokea taarifa hiyo vyema.

Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni za wizara ya afya na huduma za jamii, kwa sasa kuna visa zaidi ya 8,000 vilivyothibitishwa vya coronavirus nchini Uingereza ingawa idadi kamili ya visa huenda ikawa ni ya juu zaidi na baadhi ya wagonjwa 422 miongoni mwao wamekufa.

Mara ya mwisho mwanamfalme alionekana katika shughuli za umma tarehe 12 Machi lakini amekua akifanyia kazi zake nyumbani kwa wiki chache zilizopita ambako aliendesha mikutano ya kibinafsi na watu waliokutana nae wamefahamishwa kuhusu maambukizi aliyoyapata.

                       Mwisho.

Latest News

TANZANIA, CHINA ZAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO.
10 Jul 2020 13:10 - Grace Melleor

Tanzania na China zimeahidi kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakuwa na maendeleo  [ ... ]

Breaking News: DKT HUSSEIN MWINYI APITISHWA KUWA MGOMBEA URAIS ZANZIBAR.
10 Jul 2020 10:45 - Grace Melleor

Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM umempitisha Dkt Hussein Mwinyi kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar baada ya kupata kura  [ ... ]

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA KUFANYIKA SIMIYU TENA.
08 Jul 2020 16:48 - Grace Melleor

Serikali imetangaza kuanzia tarehe 01 hadi 08 Agosti, 2020 kutafanyika maadhimisho ya sikukuu ya wakulima Nanenane ambap [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.