Star Tv

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza juu ya ulazima wa kuachiliwa huru haraka iwezekanavyo wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa nchini Saudi Arabia.

Ismail Hania ambaye ni kiongozi wa kundi hilo amesema kuachiliwa huru kwa wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa nchini Saudi Arabia imekuwa ni dharura ya kibinadamu na kitaifa, hasa baada ya kuibuka virusi vya Corona ambavyo vinatishia uhai wa wafungwa hao.

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, Saudi Arabia inapaswa kuzingatia suala la ubinadamu na dini katika kuamiliana na faili la wafungwa wa Kipalestina.

Wakati huohuo, familia za Wapalestina wanaoshikiliwa katika magereza ya Saudi Arabia nazo zimetoa wito wa kuachiliwa huru ndugu zao na kusisitiza kwamba, tuhuma wanazokabiliwa nazo hazina msingi wowote.

Zaidi ya Wapalestina 60 wanashikiliwa katika magereza ya Saudi Arabia wakituhumiwa kuwa na uhusiana na  Harakati yaMapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS.

Baadhi ya duru zinasema kuwa, raia wa Palestina waliokamatwa nchini Saudi Arabia na wanaoshikiliwa katika magereza ya nchi hiyo wanakabiliwa na mateso mbalimbali.Hayo yanajiri huku Saudia ikiendelea kukkosolewa kwa kukiuka haki za binadamu nchinii humo.

Hivi karibuni Bi Michelle Bachelet Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa alieleza wasiwasi wake kuhusu mwenendo wa kuendelea kukamatwa wapinzani wa serikali nchini Saudi Arabia hususani wanaharakati wanawake, sanjari na kukiukwa haki za binadamu.

                         Mwisho

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.