Star Tv

Waziri wa afya nchini Kenya Mutahi Kagwe amethibitisha kisa cha mtu mmoja kutoka nchini humo kuugua ugonjwa wa Corona katika tangazo alilolitoa moja kwa moja kupitia vyombo vya habari.

Waziri Mutahi amesema kwamba mtu huyo mwenye maambikizi ya virusi vya Corona alithibitishwa kuwa ana maambukizi hayo Alhamisi usiku Machi 13,2020.

Waziri huyo amesema kisa hicho ni cha kwanza kuripotiwa nchini Kenya tangu kuzuka kwa mlipuko wa ugonjwa huo mjini Wuhan nchini China mwezi disemba mwaka jana.

Kisa hicho ni cha raia wa Kenya aliyewasili nchini humo kutoka Marekani kupitia mjini London nchini Uingereza tarehe 5 mwezi Machi 2020.

Mgonjwa huyo aligunduliwa kuwa na virusi hivyo katika maabara ya wizara ya afya nchini Kenya, huku Waziri huyo akisema kwamba mgonjwa huyo ambaye ni mwanamke yuko katika hali njema na kwamba viwango vyake vya joto vimeshuka na kuwa vya kawaida.

Aidha, Waziri Kagwe amewataka Wakenya kuwa watulivu na kuacha wasiwasi kwani serikali ya Kenya kupitia wizara ya afya itaendelea kuimarisha mikakati ili kuhakikisha kwamba hakuna usambazaji wa virusi hivyo zaidi.

Kamati ya dharura ilioanzishwa ili kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona itaendelea kutoa muongozo ili kukabiliana na ugonjwa huo hatari.

Amewahakikishia Wakenya kwamba Kenya imejiandaa vizuri ili kukabiliana na virusi hivyo tangu kisa cha kwanza kitangazwe nchini China, akiongezea kuwa serikali itatumia raslimali zake zote kukabiliana na janga hilo.

Waziri Kagwe amesema kwamba Kenya inaelekea katika wakati ambapo sekta za kibinafsi na zile za kibiashara zitalazimika kuisaidia serikali na raia katika kuchukua jukumu la kukabialana na janga hili.

                                Mwisho.

Latest News

KENYA KUTUMA NDEGE CHINA KUCHUKUA VIFAA VYA COVID-19.
06 Apr 2020 15:17 - Grace Melleor

Waziri wa Usafirishaji wa Kenya James Macharia amesema wanatarajia kutuma ndege ya Kenya Airways nchini China siku ya Ju [ ... ]

WAGONJWA WAPYA WANNE WABAINIKA KUWA NA MAAMBUKIZI NCHINI.
06 Apr 2020 14:55 - Grace Melleor

Waziri wa afya Ummy Mwalimu ametoa taarifa ya uwepo wa ongezeko la wagonjwa wanne wa Corona ambapo watu hao wamepatikana [ ... ]

WAZIRI MKUU WA UINGEREZA ALAZWA HOSPITALI MJINI LONDON.
06 Apr 2020 06:26 - Grace Melleor

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ya Downing Streeet imeeleza kuwa Waziri huyo amelazwa hospitalini ili ku [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.