Star Tv

Rais wa Marekani Donald Trump, ametangaza kuweka zuio kwa raia wa nchi za Ulaya kuingia nchini Marekani ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.

Hayo yamejiri katika hotuba ya rais Trump kwa njia ya Televisheni siku ya Jumatano, ambapo amesema safari zote za kutoka Ulaya zitazuiwa kwa siku 30 zijazo.

Visa 1,135 tayari vimethibitishwa nchini Marekani huku watu 38 wakiripotiwa kupoteza maisha Hatua ambayo inatazamiwa kuanza   kutekeleza zuio la rais Trump kuanzia usiku wa siku ya Ijumaa''. 

Tump alizungumza saa kadhaa baada ya Italia ambayo ni nchi iliyoathirika zaidi baada ya China kwa kutangaza kuchukua hatua kali amesema Umoja wa Ulaya ''umeshindwa kuchukua hatua za tahadhari.

Amesema kuahirishwa kwa safari hizo pia kutahusu biashara na usafirishaji wa mizigo kutoka Ulaya kuingia Marekani.

Pia ametangaza kutoa mkopo wa mabilioni ya dola kwa wafanyabiashara wadogo, na kutaka bunge la Congress kupitisha nafuu ya kodi ili kukabiliana na athari za mlipuko wa corona kiuchumi.

Maafisa wamesema hatari ya maambukizi ilikuwa chini, lakini hali ilibadilika baada ya ongezeko la idadi ya visa vipya vya maambukizi vilivyothibitishwa mwanzoni mwa mwezi Machi.

Jitihada za kudhibiti zimeanza na tayari vikosi vimepelekwa kwenye mji wa New Rochelle, ulio kaskazini mwa New York, ambapo mlipuko huo unaaminika kuanzia huko.

Gavana wa jimbo la Washington amepiga marufuku mikusanyiko katika kaunti kadhaa, jimbo lililo Kaskazini Magharibi ni kiini cha maambukizi nchini Marekani, kukiwa na idadi ya vifo 24 kati ya 38 nchi nzima.

Mwisho.

Latest News

TANZANIA, CHINA ZAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO.
10 Jul 2020 13:10 - Grace Melleor

Tanzania na China zimeahidi kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakuwa na maendeleo  [ ... ]

Breaking News: DKT HUSSEIN MWINYI APITISHWA KUWA MGOMBEA URAIS ZANZIBAR.
10 Jul 2020 10:45 - Grace Melleor

Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM umempitisha Dkt Hussein Mwinyi kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar baada ya kupata kura  [ ... ]

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA KUFANYIKA SIMIYU TENA.
08 Jul 2020 16:48 - Grace Melleor

Serikali imetangaza kuanzia tarehe 01 hadi 08 Agosti, 2020 kutafanyika maadhimisho ya sikukuu ya wakulima Nanenane ambap [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.