Star Tv

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amemuagiza Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani humo Kamishina Msaidizi wa Polisi Mugabo Wekwe kuwahamisha vituo vya kazi wakuu wa vituo vya Pangawe na Kingolwira.

Wakuu hao wa vituo wameamriwa kuhamishwa kwenye vituo vyao vya kazi kutokana kutuhumiwa na wakulima wa Kata za Mikese na Pangawe kupokea rushwa kutoka kwa wafugaji na hivyo kusababisha migogoro ya wakulima na wafugaji kuendelea ndani ya kata hizo.   

Loata amemuagiza Kaimu Kamanda wa Polisi Kamishina msaidizi wa Polisi Mugabo Wekwe kuwachukulia hatua wakuu wa vituo vya polisi vinavyalalamikiwa na wananchi kupokea rushwa kutoka kwa baadhi ya wafugaji na hivyo kusababisha kushindwa kutoa haki stahiki kwa wakulima.

Changamoto kubwa imetajwa kuwa katika kata za Mikese na Pangawe ambapo walio wengi wamekuwa wakipoteza mazao yao kutokana na wafugaji kugeuza mashamba hayo kuwa malisho ya mifugo yao na kisha kutoweka.

Baadhi ya wafugaji wamesema sio wote wana tabia ya kulisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima isipokuwa baadhi ndio wanafanya vitendo hivyo  vinavyowaumiza wakulima.

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa wito kwa jamii hizo mbili za wafugaji na wakulima kuzingatia sheria kutokana na jamii hizo zote mbili kutegemeana huku akiwataka watendaji mbalimbali wa serikali kuzingatia sheria na kanuni  na kuacha kujihusisha na rushwa ili kuweza kutokomeza migogoro hiyo isiyokuwa na tija kwa taifa.

                             Mwisho

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.