Star Tv

Tume ya Afya na Magonjwa ya China imesema kuwa wagonjwa wapya 889 wamethibitika kuambukizwa virusi vya Corona hadi kufikia siku ya jana.

Taarifa iliyotolewa leo imeeleza kuwa idadi hiyo imeongezeka kutoka 394 iliyoripotiwa siku moja kabla.Jumla ya idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona China bara hadi sasa imefikia 75,465.

Aidha, idadi ya watu waliokufa kutokana na virusi hivyo ni 2,236, Huku jimbo la Hubei ambako ndipo virusi hivyo vilianzia imetangaza vifo vipya 115 na kwenye mji wa Wuhan watu 99 wamepoteza Maisha kutona na virusi hivyo.

Wakati huo huo, Korea Kusini imethibitisha visa vipya 52 vya virusi vya Corona na hivyo kuifanya idadi ya watu walioambukizwa virusi hivyo kufika 156.

Idara ya kudhibiti magonjwa ya Korea Kusini, imesema visa vipya 39 vimethibitishwa katika mji wa kusini wa Daegu.

                                                                                          Mwisho.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.