Star Tv

Imeelezwa kuwa maabara ya mkemia mkuu wa serikali inakabiliwa na changamoto ya matengenezo kinga hali inayosababishwa na kutokuwa na wataalamu wenye mikataba funganishi.

 Taarifa na Piensia Rugarabamu.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa idara ya usimamizi wa kemikali Daniel William katika mkutano na waandishi wa habari wakati akieleza kuhusu mafanikio ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika kipindi cha miaka minne ya Rais Magufuli.

Amesema baadhi ya tafiti za utambuzi katika maabara hiyo zimekuwa zikichukua muda mrefu na nyingine kukwama kutokana na kutokuwepo kwa mitambo ya uchunguzi hapa nchini hali inayosababisha kuingia gharama kubwa za kununua mitambo mingine.

Kwa upande wake mkemia mkuu wa serikali Dokta Fidelis Mafumiko amesema mammlaka hiyo ipo mbioni kuanzisha kanzi data mpya ya taifa hali itakayosaidia kuongeza uwezo wa mammlaka hiyo kufanya utambuzi wa haraka wa watu waliofanya uhalifu.

Kwa mujibu wa mkemia mkuu, maabara hiyo imefanikiwa kufanya majaribio ya vinasaba kwa asilimia 100, pamoja na kufanya uchunguzi wa vinasaba kwa mambo yanayotokana na majanga ambapo imewataka wananchi kupuuzia taarifa sizizo za kweli juu ya gharama za upimaji vinasaba na kueleza gharama halisi ni shilingi laki moja kwa mtu mmoja.

                                                                                                         Mwisho.

 

Latest News


Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.