Star Tv

Kesi ya jinai inayomkabili mwalimu Focus Mbilinyi dhidi ya Jamhuri kwa tuhuma za Kumpiga mwanafunzi na kumsababishia ulemavu imeendelea kusikilizwa katika mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Njombe  ambapo mashahidi wawili wa upande wa jamhuri walifika mahakamani hapo kuwasilisha ushahidi wao.

Taarifa zaidi na Dickson Kanyika Kutoka njombe.

Kesi hiyo namba 141 ya mwaka 2019 inayomkabili Aliyekuwa mwalimu ya Shule ya Msingi Madeke Focus Mbilinyi dhidi ya jamhuri imeendelea kusikilizwa katika mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya njombe ikiwa chini ya Hakimu Irvan Msaki na wakili wa serikali akiwa ni Elizabeth Malya.

Mahakama iliwapokea mashaidi wawili Given Nyanginywa ambae ni mwanafunzi mwenza wa mtoto Hosea Manga pamoja na Daktari Silvery Mwesige waliwasili mahakamani kutoa ushahidi juu ya mtoto Hosea Manga ambae kwa sasa hawezi tena kurejea kwenye hali yake ya awali kwa mujibu wa ripoti ya madaktari.

Shahidi wa Kwanza Given Nyanginywa aliambia mahakama kwamba mnamo tarehe 21 mwezi Machi mwalimu focus mbilinyi alitoa hesabu kumi na baadae alitoa adhabu kwa wanafunzi wote waliokosa hesabu hizo na miongoni mwa wanafunzi walioadhibiwa siku hiyo ni pamoja na mtoto Hosea Manga ambae alipigwa viboko kumi huku akiwa amening’inizwa dirishani kwa mtindo wa miguu juu kichwa chini.

Aliendelea kuiambia mahakama kuwa baada ya Hosea kupigwa viboko hivyo alianguka chini na kushindwa kunyanyuka.

Kwa Upande wake Shahidi namba 4 Daktari Silvery Mwesige aliambia mahakama kwamba mtoto Hosea manga walimpokea Takribani wiki mbili baada ya kupata matatizo akitokea hospitali ya Ikonda.

Mwesige aliambia mahakama pia baada ya vipimo kufanyika walibaini kuwepo kwa mgandamizo chini ya uti wa mgongo uliopelekea kupishana kwa pingili za uti wa mgongo na kusababisha mfumo wa damu kushindwa kupenya kwenda sehemu za chini ya mwili wa mtoto Hosea yaani kiunoni hadi miguuni.

Licha Ushahidi huo kuwasilishwa Mahakamani hapo pamoja na kielelezo cha ripoti ya matibabu ya mtoto Hosea mawakili upande wa utetezi walipinga kielelezo hicho kwa madai ya kwamba ripoti hiyo ya matibabu imewasilishwa na mtu ambae hajaiandaa pingamizi ambalo mahakama imelitupilia mbali.

Kesi hiyo imesikilizwa kwa zaidi ya masaa sita, na  mwisho mahakama ilikubali kielelezo hicho kilichowasilishwa na daktari Silvery Mwesige kutoka hospitali ya taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa MOI , na baadaye mahakama iliamua kuahirisha kwa kesi hiyo hadi disemba 2 mwaka huu.

                                                                                      Mwisho

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.