Star Tv

Wanafunzi saba wamekufa na wengine 57 wamejeruhiwa baada ya jengo la darasa moja kuanguka katika shule moja ya msingi katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Msemaji wa serikali ya Kenya, Kanali Cyrus Oguna, amewaambia waandishi habari kwamba jengo hilo limeanguka mapema leo asubuhi katika shule ya Precious Talent Academy kwenye eneo la Dagoretti. Majeruhi wa kwanza waliondolewa na kupelekwa katika zahanati ya Kanisa Katoliki iliyo karibu na shule hiyo kwa kutumia pikipiki, kwa sababu magari ya kubeba wagonjwa yalifika baada ya saa moja. Shirika la Msalaba Mwekundu limeandika katika mtadao wake wa Twitter kwamba limefungua dawati la kutoa taarifa na litatoa msaada wa huduma za kisaikolojia. Mkuu wa shule hiyo, Moses Wainaina Ndirangu amesema huenda jengo hilo limeanguka kutokana na ukarabati unaoendeleza katika mifumo ya maji taka kwenye upande mmoja wa madarasa.

CHANZO: Idhaa ya Kiswahili DW

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.