Star Tv

Uganda imeachana na mradi wa kujenga bwawa la kufua umeme katika maporomoko ya maji ya Marchison.

Mradi huo ulikuwa ukikosolewa sana na walinzi wa mazingira na wadau kadhaa wa sekta ya utalii. Serikali ya Uganda inaashiria mradi huo wa umeme wenye uwezo wa kutoa megawatt 360 "ungechafua mandhari na kuvuruga mfumo wa ikolojia na kwa namna hiyo ungeharibu pia shughuli za utalii. Zaidi ya watalii 100.000 wanatembelea kila mwaka maporomoko ya Murchison ili kujionea maajabu ya dunia. Kwa mujibu wa waziri wa utalii Ephraim Kamuntu serikali imepitisha uamuzi huo kaatika kikao cha hivi karibuni cha baraza la mawaziri. Uchumi wa Ugaanda unanawiri kwa mujibu wa benki kuu ya dunia ukuaji wa kiuchumi unafikia asili mia sita kwa mwaka nchini humo.

CHANZO: Idhaa ya Kiswahili DW

Latest News

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Urusi Kuchagiza Maendeleo Afrika kupitia Nishati ya Nuklia na Madini ya Urani
12 Aug 2023 10:07 - Kisali Shombe

ROSATOM, taasisi ya nishati ya nyuklia ya serikali ya Urusi ambayo iliwaalika zaidi ya waandishi wa habari 15 kutoka nch [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.