Baraza la kijeshi linalotawala Sudan limekiri kwamba vikosi vya usalama vilikiuka sheria wakati wa kuwatawanya waandamanaji nje ya makao makuu ya jeshi katika mji mkuu wa Khartoum wiki iliyopita.
Msemaji wa baraza hilo la mpito, Jenerali Shamseddin Kabashi, aliwaambia waandishi wa habari kuwa uchunguzi unaendelea na kwamba maafisa kadhaa wa kijeshi wamewekwa kizuizini kwa madai ya kukiuka maelekezo ya viongozi wa kijeshi lakini jenerali Kabashi hakufafanua zaidi. Kulingana na waandaaji wa maandamano ya Sudan watu wapatao 100 waliuawa katika mji mkuu wa Khartoum wakati wa makabiliano na vikosi vya usalama. Waandamanaji pia wamesema zaidi ya miili 40 iliopolewa katika Mto Nile.
CHANZO: Idhaa ya Kiswahili DW