Tanzania imeendelea kuweka juhudi za kuimarisha miundombinu ya usafirishaji ikiwemo kuimarisha bandari ya Dar es Salaam na Mtwara, kujenga bandari kavu na kukamilisha ujenzi wa barabara ya Mtwara-Mbambabay ambayo itawawezesha wafanyabiashara wa Malawi kutumia bandari ya Mtwara.
Hayo yamejiri katika ziara ya TPA pamoja na wadau mbalimbali kama TATOA, TRA, TAZARA, TAFFA, TICTS, DCG, katika kukagua miundombinu ya usafirishaji wa mizigo ya wafanyabiashara wa Malawi kuitikia maelekezo yaliyotolewa na Rais, DK; John Magufuli wakati wa ziara yake Aprili 24, mwaka huu nchini Malawi. Rais DK; Magufuli aliagiza TPA pamoja na wadau wa sekta ya usafirashaji na wadau wengine kutatua kero zinazowakabili wafanyabiashara wa Malawi ili waweze kutumia bandari ya Dar es Salaam. Aidha kujengwa kwa bandari kavu na kukamilishwa kwa ujenzi wa barabara ya Mtwara-Mbambabay kutawezesha wafanyabiashara wa Malawi kutumia bandari ya Mtwara ambayo iko umbali mfupi wa kilometa 820.