Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amewasili mjini Kharotum, Sudan kusimamia mazungumzo kati ya baraza la kijeshi na viongozi wa waandamanaji kufuatia hatua kali za kijeshi dhidi ya waandamanaji wiki hii.
Kulingana na shirika la habari la AFP Abiy ataongoza mikutano kati yake na watawala wa kijeshi na baadaye atakutana kwa mazungumzo na viongozi wa waandamanaji lakini kwa nyakati tofauti. Ziara yake inakuja baada ya Umoja wa Afrika wenye makao yake Addis Ababa Ethiopia, kusimamisha uanachama wa Sudan kufuatia mzozo wa kisiasa nchini humo. Kulingana na jumuiya ya madaktari nchini Sudan, watu 113 wameuawa kufuatia hatua hizo kali za kijeshi zilizoanza kuchukuliwa siku ya Jumatatu kwa lengo la kuwatawanya waandamanaji.
CHANZO: Idhaa ya Kiswahili DW