Uongozi wa Hospital ya rufaa ya mkoa wa Mara umelazimika kufunga kamera maalumu katika maeneo yote ya hospitali hiyo ili kukabiliana na matatizo ya wizi wa vifaa tiba na vitisho toka kwa ndugu wa wagonjwa kuwapiga wauguzi pindi wanapotoa huduma.
Mganga mfawidhi wa hospital ya rufaa ya mkoa wa Mara Dr Joakim Eyembe amefanya mazungumzo na wauguzi baada ya kusikiliza kero zinazowakabili juu ya vitisho toka kwa ndugu wa wagonjwa na wizi wa vifaa tiba amewaondoa hofu kwa kuwaambia tayari kamera zimefungwa kila sehemu. Dr Eyembe ameongeza kuwa wameamua kuajiri kampuni maalumu ya ulinzi ili kuweza kukabiliana na tatizo la wizi wa vifaa tiba ufanywao na vijana wanaoingia kwa kupitia katika uzio. Hayo yamejiri katika kilele cha siku ya wauguzi duniani kilichofanyika katika viwanja vya hospital hiyo huku wauguzi wakitoa huduma mbali mbali kwa wagonjwa.