Star Tv

Usalama umeimarishwa katika mji wa Christchurch nchini New Zealand Jumatatu ya leo, wakati shule na biashara zikifungua milango kwa mara ya kwanza tangu shambulizi la kigaidi dhidi ya miskiti miwili katika mji huo, ambamo watu 50 waliuawa.

Mshukiwa wa shambulizi hilo, Brenton Tarrant ambaye anajinadi kuwa mfuasi sugu wa sera za kuwaenzi Wazungu anaendelea kushikiliwa rumande, wakati uchunguzi ukifanyika katika nchi kadhaa, na New Zealand ikiandaa kikao maalum cha baraza la mawaziri kujadili hatua za kuchukuliwa kuhusiana na shambulizi hilo. Makaburi yamechimbwa tayari kwa mazishi ya baadhi ya wahanga wa shambulio hilo la kigaidi baadaye leo. Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern amezishinikiza kampuni za mitanado ya kijamii kutoa maelezo juu ya namna mshambuliaji alivyoweza kurusha moja kwa moja mitandaoni shambulizi lake kwa muda wa dakika 17, na vidio ya shambulizi hilo kuenea mitandaoni kwa masaa kadhaa. Amesema pia kuwa nchi yake itaimarisha sheria ya umiliki wa bunduki.

Chanzo: DW Swahili

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.