Star Tv

Mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda ambaye ni mwalimu wa chuo kikuu Christopher Kayumba ameshikiliwa kwa madai ya ubakaji.

Ofisi ya uchunguzi nchini humo imesema imemaliza kufanya uchunguzi na imeshakabidhi mashtaka yake ili yaweze kusikilizwa.

Kiongozi huyo ambaye ni wa chama cha jukwaa la demokrasia yaani Rwandan Platform for Democracy (RPD) alishutumiwa kwa madai ya ubakaji siku chache baada ya kuzindua chama chake.

Kayumba amekanusha madai hayo dhidi yake na kusema wana nia ya kumuharibia taswira yake kwa umma pamoja na ya chama chake.

Aidha, miongoni mwa watu wanaomshutumu ni mwanafunzi wake wa zamani.

#ChanzoBBCSwahili

Latest News

UFARANSA YAZINDUA MAGARI YA UMEME HAPA NCHINI.
20 Oct 2021 15:31 - Grace Melleor

Waziri wa Biashara na uchumi nchini Ufaransa Franck Riester amezindua magari ya umeme yaliyoundwa na kampuni ya E-Motion [ ... ]

UHITAJI WA NYAMA WAONGEZEKA NCHINI.
20 Oct 2021 15:23 - Grace Melleor

Serikali imesema malalamiko yaliyojitokeza hivi karibuni ya kupanda kwa bei ya nyama nchini yanaashiria ukuaji wa sekta  [ ... ]

UGANDA YAZINDUA GARI LA KIVITA LILILOUNDWA NCHINI HUMO.
19 Oct 2021 18:03 - Grace Melleor

Jeshi la Uganda limezindua gari la kivita lililoundwa nchini humo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.