Profesa Lubaina Himid ni mzaliwa wa Zanzibar ambaye ni mtanzania ametangazwa kuwa mshindi wa 'Turner Prize 2017'katika tuzo kubwa za Sanaa nchini Uingereza.
Himid amekuwa mshindi mwenye umri mkubwa wa miaka 63 kwenye tuzo hizo.
Tuzo hizo zilikuwa wazi kwa watu walio na umri wa chini ya miaka 50,lakini sheria hiyo ilibadilishwa mwaka huu.
Majaji wamempa Tuzo kwa maonesho matatu yaliyofanyika Oxford, Bristol na Nottingham ambapo waliisifu kazi yake ambayo inaangazia Afrika duniani kote pamoja na ubunifu wa mtu mweusi jambo ambalo wameliita namna nzuri ya ubunifu.
Profesa Himid ambaye ni mwanamke wa kwanza mweusi na mtu mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kutwaa Tuzo hiyo amesema atatumia tuzo ya fedha ya dola elfu thelathini na tatu ($33,000) alizozipata kuwasaidia wasanii wachanga kuweza kuonesha kazi zao.
Kwa hisani ya BBC