Mwanamke raia wa Misri ambaye aliaminiwa kuwa mtu mwenye uzani mkubwa zaidi duniani amefariki kwenye hospitali moja katika umoja wa falme za kiarabu
Eman Ahmed Abd El Aty alikuwa amepelekwa nchini India kufanyiwa upasuaji wa kupunguza uzito wa mwili.
Vyombo vya habari viliripoti kuwa alikuwa amepunguza uzito kwa kilo 300 kutoka kwa uzito wa kilo 500 lakini akafariki kutokana matatizo mengine ya kiafya.
Taarifa za hospitali zinasema kwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 37 alikuwa na ugonjwa wa moyo na matatizo ya figo.