Ndoto na Shauku ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kuweka Mazingira Bora ya Walimu inakaribia kutimia ambapo leo amefanya Uzinduzi wa Zoezi la Kuezeka Mabati kwenye ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu Dar es salaam na kupokea hundi ya Shilingi Million 50 kutoka kampuni ya mawasiliano ya Halotel iliyoguswa na kampeni ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu Dar. Ujenzi wa Ofisi hizo 402 ni jitiada za RC Makonda kuboresha Mazingira ya Walimu baada ya kufanya kikao na Wakuu wa Shule na kugundua walimu wanafanya kazi katika Mazingira Magumu ikiwemo kufanya kazi zao Chini ya Miti na ukosefu wa Vyoo. Kama ilivyo kawaida yake kutoa Majibu kwenye changamoto RC Makonda aliamua kuanza kampeni ya Ujenzi wa Ofisi 402 za walimu Dar es salaam zenye hadhi ambapo ndani yake kuna Ofisi ya Mwalimu Mkuu, Mwalimu Mkuu Msaidizi, Ofisi ya Walimu wote, Vyoo, Bafu, Jiko, Ofisi ya Mhasibu, Chumba cha kuhifadhi Nyaraka, Chumba cha kubadilisha Nguo, Mapokezi, Ukumbi wa Mkutano na vifaa vya kisasa kutoka Marekani ikiwemo Meza, Viti, Computer, AC na TV. RC Makonda amesema ndoto na shauku yake ni kuona Elimu Bora inatolewa ili kusaidia Taifa kuwa na Wataalamu wa kutosha kuepuka kuchukuwa Wataalamu kutoka Nje ya Nchi na ili kufikia huko ni lazima Walimu wawekewe Mazingira Bora ya kufanya kazi kwakuwa tayari Rais Magufuli ameshaonyesha Dira kwa kutoa Elimu Bure ili kumwezesha Mtoto wa Maskini kuwa na utajiri na kunufaika na rasilimali za Nchi hii. Aidha Makonda ameishukuru kampuni ya Mawasiliano ya Halotel kwa kuchangia kiasi cha Shilingi Million 50 kama sehemu ya awamu ya kwanzaa ambapo wameahidi kuongeza Million 50 nyingine. RC Makonda amesema katika awamu ya kwanza watakabidhi Ofisi 100 na kuwaomba Wananchi kushirikiana na Serikali kwa kuendelea kuchangia kampeni hiyo ili kuwawezesha Walimu kufanya kazi katika mazingira mazuri. Nao baadhi ya Walimu walioshiriki uzinduzi huo wamemshukuru RC Makonda kwa kuwajengea ofisi hizo zenye hadhi ya kipekee ambazo zinaenda kumaliza changamoto ya muda mrefu kufanya kazi chini ya miti,madarasani pamoja na ukosefu wa vyoo. Pia Walimu hao Wamemshukuru RC Makonda kwa kuwawezesha kusafiri Bure kwenye usafiri wa Umma na kupata Viwanja vya Bei nafuu. TUSHIRIKIANE KWA PAMOJA KUWEKA MAZINGIRA BORA YA ELIMU DAR ES SALAAM

Latest News

Diamond ahojiwa na Polisi kuhusu picha za mitandaoni
17 Apr 2018 12:43 - Joseph Musyoka

Mwanamziki maarufu wa Bongo fleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz amekuwa akihojiwa na Polisi kuhusu video il [ ... ]

Mwanasiasa wa Kenya Kenneth Matiba amefariki
16 Apr 2018 11:22 - RobinLeah Madaha

Mwanasiasa shupavu wa upinzani nchini Kenya Kenneth Stanley Njindo Matiba amefariki.

Mshairi kufungwa jela kwa kuhamasisha umoja Somalia
16 Apr 2018 09:23 - RobinLeah Madaha

Mahakama ya serikali iliyojitenga ya Somaliland imemfunga jela miaka mitatu ,msichana anayeimba mashairi kwa kosa la kuh [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.