Star Tv
Maafisa wa Afya nchini Syria katika maeneo ya waasi yaliyozingirwa kaskazini mwa Ghouta wamesema watu kadhaa wamedhurika kutokana na na dalili zinazoonesha kuathiriwa na gesi ya Klorini, wakati wa mashambulizi yaliyokuwa yakifanywa na majeshi yanayounga mkono serikali. Taaarifa uiliyotolewa na Wizara ya Afya inayoendeshwa na wapinzani imesema waathirika, madereva wa magari ya kubeba wagonjwa na watu wengine wameripotiwa kuvuta gesi hiyo ya Klorini baada ya mlipuko. Watu 18 wanatibiwa kwa kuwekewa Oxygen. Mkazi mmoja katika eneo la mashariki ya Ghouta ameiambia BBC kuna mtoto pia ameathirika. Dokta Mohammed Khatoub aliyeko Uturuki, ambaye anatokea katika mji wa Ghouta ameelezea uthibitisho wa hospital wanakotibiwa majeruhi hao, kwamba wameathiriwa na gesi hiyo. Hata hivyo Serikali ya Syria siku zote imekuwa ikikanusha kutumia silaha za kemikali. Mashambulizi ya ardhini yalipamba moto jana Jumapili, licha ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutaka kusimamishwa kwa mapigano hayo.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.