Star Tv
Huduma za serikali ya Marekani zimekwama baada ya bunge la Congress kushindwa kupitisha mkakati muhimu wa bajeti yake kwa wakati unaofaa. Wabunge walitumai kwamba watapitisha matumizi mapya kabla ya muda wa kufadhili bajeti hiyo kukamilika. Lakini seneta wa Republican Rand Paul alimaliza matumaini ya kupigwa kwa kura ya haraka wakati alipoitisha mjadala bungeni kuhusu marekebisho ya matumizi. Mnamo mwezi Januari , kisa kama hicho cha kushindwa kupitisha matumizi ya serikali katika wakati unaofaa kilisababisha serikali kuwa na mkwamo wa siku tatu. Hatahivyo wafanyikazi wa serikali wameombwa kutumia maajenti wa nyumbani ili kupata ,mwelekeo kuhusu ni lini watarudi kazini. Mabunge yote ya seneti na lile la uwakilishi ni sharti yaidhinishe matumizi hayo ya miaka miwili. Mkwamo huo ulitarajiwa ikiwa imesalia saa moja kabla ya muda kukamilika wakati bunge la seneti lilipopiga kura ya mapumziko. Lakini licha ya kuchleweshwa ,bunge hilo linatarajiwa kupigia kura matumizi hayo. Bunge la uwakilishi halitapiga kura yoyote hadi pale bunge la seneti litakapoidhinisha matumizi hayo. Haijulikani ni vipi bunge la Congress litaendelea na vile huduma za umma zitakavyoathirika. Hatua hiyo itasababisha kupanda kwa matumizi hadi $300bn (£215bn) - Kitu ambacho seneta Paul anasisitiza hawezi kuunga mkono.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.