Star Tv

Aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama ameonya kuhusu matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii wakati wa mahojiano yasiyo ya kawaida tangu aondoke madarakani mwezi Januari.

Alionya kuwa vitendo kama hivyo vinachanganya uelewa wa watu katika masuala magumu na kusambaza uvumi.Mrithi wake Donald Trump ni mtumiaji mkubwa wa Twitter lakini Obama hakumtaja jina.

Obama alisema wale walio katika nyadhifa za uongozi wanastahili kuwa waangalifu wakati wanaandika katika mitandao.

Alielezea wasi wasi kuhusu siku za usoni ambapo ukweli utapotoshwa na watu watakuwa wakisema, watakuwa wakisoma na kusikiliza vitu ambavyo vitakuwa vikiridhisha maoni yao.Bw. Trump amelaumiwa kwa kutumia mtandao wa Twitter kupindukia licha ya yeye kusisitiza kuwa inamruhusu kuwasiliana moja kwa moja na watu wa Marekani.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.