Star Tv

Tetemeko la ardhi limetokea katika eneo la la mpaka wa Iran naIraq na kuua zaidi ya watu 400 na kujeruhi zaidi ya watu 7000.

Makundi Ya ukoaji yanaendelea na uokoaji yanaendelea na jitihada za kutafuta manusura waliofunikwa na vifusi Licha ya hospitali kuu ya mkoa huo kuharibiwa vibaya na kushindwa kuhudumia wagonjwa ipasavyo.

Tetemeko hilo ndilo baya zaidi kutokea duniani mwaka huu. Watu wengine walioawa walikuwa kwenye mji ulio magharibu mwa Iran wa Sarpol-e-Zahab ulio umbali wa kilomita 15 kutoka mpaka na sehemu zingine za mkoa wa Kermanshah.

Mwanamke mmoja na mtoto waliondolewa kutoka kwa vifusi wakiwa hai kwenye mji huo, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Iran.Huduma za maji na umeme zimekatwa katika miji mingine na baada ya majengo kuporomoka watu walilazimika kulala nje kwenye baridi.

Shirika moja la utoaji misaada lilisema kuwa watu 70,000 wanahitaji makao baada ya tetemeko hilo, na kuna ripoti kuwa maelfu ya watu huenda wakalala nje kwa usiku wa pili.

Maafisa nchini Iran wanasema kuwa watu 413 wameuawa nchi humo. Baadhi ya wanajeshi na walinzi wa mpaka ni kati ya wale waliouawa.

Nchini Iraq watu 9 waliuawa kwa mujibu wa msemaji wa shirika la msalaba mwekundu. Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini humo ilisema kuwa watu 500 walijeruhiwa huko na tetemeko hilo lilisikika huko Irbil, Sulaimaniya, Kirkuk, Basra na mji mkuu Baghdad.

Kwa hisani ya BBC.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.