Klabu ya Yeovil Town inayocheza ligi ya daraja la tatu, ambayo ndiyo klabu ya ngazi ya chini zaidi iliyosalia katika Kombe la FA msimu huu, imepangwa kukutana na mabingwa mara 12 wa kombe hilo Manchester United raundi ya nne.
Tottenham pia watakutana na klabu ya League Two, Newport County. Viongozi wa Ligi ya Premia Manchester City wamepangwa kukutana na mshindi kati ya Cardiff City na Mansfield. Nottingham Forest, ambao waliwaondoa mabingwa watetezi Arsenal Jumapili watakutana na wenzao wa ligi ya Championship Hull City.
Mechi za raundi ya nne zitachezwa wikendi ya 26-29 Januari.
Kwa hisani ya BBC.