Takriban miaka mitano baada ya kujitoa katika jumuiya ya madola leo Gambia inajiunga upya. Sherehe inafanyika leo Alhamisi katika makao makuu ya jumuiya hiyo mjini London kuidhinisha kurudi kwa nchi hiyo kama taifa mwanachama wa jumuiya ya madola. Mnamo Februari 2017, rais mpya aliyechaguliwa Adama Barrow aliomba nafasi ya taifa lake kurudi kuwa mwanachama, na mwezi Desemba bunge nchini humo liliidhinisha ombi hilo la kurudi katika kundi hilo linalojumuisha mataifa yaliokuwa chini ya ukoloni wa Uingereza. Gambia ilijiondoa katika jumuiya hiyo mnamo Octoba 2013. Rais wa zamani Yahya Jammeh aliishutumu jumuiya hiyo kwa kuwa anachokitaja "taasisi ya ukoloni mambo leo". Aliishutumu Uingereza kwa kuwaunga mkono wapinzani wake wa kisiasa. Yahya Jammeh alilitawala taifa hilo dogo la Afrika magharibi kwa miaka 22. Alishindwa katika uchaguzi mkuu mnamo Desemba 2016 lakini akajaribu kufuta matokeo ya uchaguzi huo. Ilichukua wiki kadhaa za majadiliano na tishio la jeshi kuingilia kati kumlazimisha aachilie madaraka. Baada ya Afrika kusini, Pakistan na Fiji, sasa Gambia inakuwa nchi ya nne kurudi katika jumuiya ya madola. Afrika kusini ilitangaza kujitoa katika jumuiya hiyo mnamo Mei mwaka 1961 baada ya kupitisha sheria ilioifanya nchi hiyo kuwa Jamhuri na kusitisha utawala wa malkia. Ilijunga upya miaka 33 baadaye mnamo 1994 baada ya kumalizika kwa ubaguzi wa rangi nchini. Mnamo 2008 Jumuiya ya madola ilikubali kuirudisha Pakistan mwaka mmoja baada ya kuusitishauwanachama wake kufuatia hatua ya kiongozi aliyekuwepo Pervez Musharaf kuidhinisha hali ya hatari na kuwazuia maelfu ya wanaharakati wa upinzani. Gambia ilijiunga na jumuiya ya madola kwa mara ya kwanza mnamo 1965, muda mfupi tu baada ya kupata uhuru kutoka kwa Uingereza. Ombi la Gabon mwaka jana kurudi katika jumuiya ya madola liliitikiwa na wengi, na sasa Gambia imerudi rasmi na imealikwa kuhudhuria mkutano wa viongozi wa serikali wa jumuiya ya madola huko London mwezi Aprili. Kwa sasa kuna mataifa 53 katika jumuiya hiyo. Kwa hisanio ya BBC.

Latest News

Amtumia ndugu yake kutoroka jela
14 Feb 2018 14:15 - Mohamed Mnzava

Mamlaka nchini Peru zimemkamata mfungwa zaidi ya mwaka mmoja tangu atoroke jela kwa kumuacha ndugu yake pacha katika naf [ ... ]

Ukame Cape Town umekuwa 'Janga la kitaifa'
14 Feb 2018 14:05 - Mohamed Mnzava

Afrika kusini imetangaza ukame unaoshuhudiwa Cape Town - mji unao elekea kuishia bila ya hata tone la maji - kuwa janga  [ ... ]

Waziri Mwigulu azungumzia kampeni kuhusishwa na tukio la Mbunge Lissu
14 Feb 2018 13:51 - Mohamed Mnzava

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewataka wanasiasa kuacha kutumia kesi ya kuumwa kwa Mbunge wa Singida [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.