Jaji Mstaafu Mark Bomani ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Tanzania, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Septemba 11, 2020, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha, amethibitisha na kusema kuwa Jaji Mstaafu Mzee Bomani alilazwa hospitalini hapo kwa siku 24.
"Jaji Mstaafu amefia hapa Muhimbili, amefariki majira ya saa 4:00 usiku wa kuamkia leo, na alikuwa hapa hospitalini kwa siku 24", amesema Aligaesha.
Jaji Mstaafu Mark Bomani alizaliwa 22 Oktoba 1943, Wete, Pemba-Zanzibar alikuwa ni mwanasheria mkuu kwa mwaka 1965 hadi 1976 wakati wa Utawala wa Rais wa Kwanza wa Tanzania, Julius Kambarage Nyerere.
Baada ya Jaji Bomani, alifuatiwa na Joseph Warioba na Jaji huyo amefariki akiwa ni Jaji mstaafu ambaye ana kampuni binafsi ya sheria.