Star Tv

Ratiba ya mikutano 5 ya mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu, iliyopangwa kufanyika leo Septemba 10 mkoani Pwani, imevurugika.

Chanzo cha mikutano hiyo kuvurugika ni baada ya helkopta aliyokuwa aitumie kufika katika maeneo hayo, kuzuiliwa kwa kukosa kibali na Mamlaka ya Anga nchini, muda mfupi kabla ya kurukakama alivyoeleza Mkuu wa Idara ya Habari na MAwasiliano wa chama hicho..

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Tumaini Makene ametoa taarifa ya kuvurugika kwa mkutano huo ambapo ameeleza kuwa;"Helkopta hiyo kuruka zilitolewa kwa Ofisa Mnadhimu wa Kampeni, Amani Golugwa, wakati msafara Lissu ukielekea kupanda ndege baada ya kumaliza taratibu zote za ukaguzi wa kiusalama Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) terminal I.".

Aidha, Makene amesema Ofisa wa Mamlaka ya Anga aliyewasilisha taarifa hiyo wakati msafara wa mgombea huyo wa Urais ulipangwa kuelekea Bagamoyo, Chalinze, Mlandizi na Kibaha, wakati kibali chake kiliombwa tangu jana.

Kutokana na hatua hiyo, chama hicho kimelazimika kutafuta njia mbadala ili Mgombea Urais Tundu Lissu msafara wake, aweze kuendelea na ratiba ya mikutano kwa kadri inavyowezekana.

Latest News

JAJI MKUU WA KENYA AMSIHI RAIS KENYATTA KULIVUNJA BUNGE.
22 Sep 2020 10:22 - Grace Melleor

Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, amemshauri rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, kulivunja bunge la kitaifa na lile la Sene [ ... ]

“IRAN ITAJIBU VIKALI UONEVU WA MAREKANI"- Rais Hassan Rouhani.
21 Sep 2020 11:51 - Grace Melleor

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema Marekani imeshindwa katika juhudi zake za kuiwekea tena vikwazo nchi hiyo baada ya w [ ... ]

UGANDA YAENDELEA KULEGEZA VIZUIZI DHIDI YA CORONA.
21 Sep 2020 06:31 - Grace Melleor

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kuwa shule na taasisi zingine za elimu ya juu, zitafunguliwa tena kuanzia mwez [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.