Star Tv

Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania Plc, imeilipa Serikali ya Tanzania, shilingi 32.9 bilion kama gawio na mchango maalum wa maendeleo baada ya kupata faida katika Mwaka wa Fedha 2019/20.

Mfano wa Hundi mbili za fedha hizo Fedha hizo ziliwasilishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Airtel Tanzania Plc, Bw. Gabriel Malata na kupokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango ambaye pia ndiye mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Doto James, Jijini Dodoma.

Akikabidhi hundi hiyo, Bw. Malata alisema katika kiwango hicho cha shilingi bilioni 32.99, shilingi bilioni 18.99 ni gawio na shilingi bilioni 14 ni mchango maalum wa maendeleo kwa Serikali baada ya Kampuni hiyo kupata faida ya bilioni 38.5 kwa mwaka unaoishia Disemba 2019/2020.

Akielezea mafanikio yaliyosababisha Kampuni yake kutoa gawio nono na michango ya maendeleo ya shilingi bilioni 1 kila mwezi, Bw. Gabriel Malata alisema licha ya uwekezaji mzuri katika upanuzi wa mtandao, idadi ya wateja imeongezeka kutoka milioni 11.4 Machi 2019 mpaka 13.3 milioni Machi 2020 na kwa sasa umiliki wa soko ni asilimia 27 kwa taarifa ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Pia ameeleza kuwa Airtel Tanzania Plc imetoa ajira za moja kwa moja zaidi ya 500 huku wanafanyakazi wa kigeni wakiwa saba tu na kupitia kampuni hiyo, Watanzania 350,000 wamejiajiri kwa kuuza huduma za kampuni ya Airtel Tanzania Plc kama vile kuuza vocha, mawakala wa Airtel Money hivyo kuchangia maendeleo ya uchumi kwa kulipa ushuru kwa Serikali

Kampuni hiyo imethibitisha kuwa imeunga mkono maendeleo ya serikali kama elimu na afya, Airtel pia imetoa 2.3 bilioni kwenye ujenzi wa Hospitali mkoani Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James alisema tukio hilo la Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel kutoa gawio na mchango wa maendeleo wa shilingi bilioni 32.99 ni la kihistoria baada ya Serikali na Kampuni hiyo kuingia makubaliano maalumu ya kiutendaji na kiumiliki yaliyofanyika mwaka 2019.

Bw.James ameipongeza Kampuni ya Airtel Tanzania kwa kutoa kiasi hicho kikubwa cha gawio cha shilingi bilioni 18.99 na kiasi kingine cha shilingi bilioni 14 zinazotokana na mchango wa Kampuni hiyo kwa Serikali ambapo inatoa shilingi bilioni 1 kila mwezi kuanzia mwaka jana na itakuwa ikifanya hivyo katika kipindi cha miaka mitano ambapo jumla ya shilingi bilioni 60 zinatarajiwa kupatikana.

Mashirika ambayo Serikali inamiliki hisa yametakiwa kuiga mfano wa Kampuni ya Airtel ili fedha zinazopatikana zichangie shughuli mbalimbali za maendeleo ya nchi ikiwemo kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo, kuboresha huduma za jamii kama vile afya, elimu na maji kwa Watanzania wote.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.