Star Tv

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema leo kinatarajia kuishangaza dunia wakati kikizindua kampeni za uchaguzi mkuu wa urais, ubunge na udiwani katika Uwanja wa Jamhuri.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, alisema utakuwa uzinduzi wa aina yake ambao haujawahi kufanywa na chama chochote.

“Uwanja wa Jamhuri tutakuwa na jambo letu, tutaisimamisha dunia... Halitakuwa jambo la kubahatisha, utakuwa uzinduzi babu kubwa,” alisema Polepole na kuongeza:

Polepole alisema kuanzia saa 7:00 mchana shughuli rasmi za kampeni zitaanza na kwamba wanatarajia uwanja kufurika, hivyo kutafungwa Televisheni nje ya uwanja ili kuwawezesha Watanzania watakaoshindwa kuingia uwanjani kutazama.

Aidha, Polepole alisema katika uzinduzi huo, wasanii mbalimbali watatumbuiza wakiwamo Diamond, Ali Kiba, Harmonize, Masanja, Hamza Kalala, Mrisho Mpoto, Lavalava, Beka Flavor, Shilole, G-Nako, Nandi, Maua Sama, Joti na wengineo.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipanga Agosti 26, Ambapo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilizindua kampeni zake Agosti 28 katika uwanja wa Mbagala Zakhiem jijini Dar es Salaam, huku Chama Cha Mapinduzi kikizindua kampeni zake leo agosti 29 katika uwamja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.