Star Tv

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imewaagiza wamiliki wa ndege ndogo zisizo na rubani (drones) kuhakikisha ndege hizo zimesajiliwa ifikapo Agosti 28, 2020.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA imeeleza kuwa agizo hilo ni utekelezaji wa kanuni za kiusalama za kudhibiti matumizi ya ndege zisizo na rubani za mwaka 2018 na kuwa yeyote atakayekiuka atachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa mujibu wa kanuni hizo, mtu au kampuni inayotaka kumiliki ndege hizo inatakiwa kuomba kibali TCAA kabla ya kuingiza na kusajili.

Aidha, wamiliki wanatakiwa kuomba kibali TCAA na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi na serikali za mitaa wakati wa matumizi.

TCAA imewaelekeza wamiliki wa ndege hizo kufika katika ofisi zao za kanda kwenye mikoa mbalimbali pamoja na makao makuu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya usajili.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.