Star Tv

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ametangaza siku 07 za maombolezo ya kitaifa kuanzia Ijumaa ya leo Julai 24, kufuatia kifo cha rais mstaafu wa awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa kilichotokea Dar es Salaam.

Rais amesema kuwa katika kipindi chote bendera zitapepea nusu mlingoti.

Aidha Rais Magufuli amewaomba Watanzania wote kuendelea kuwa watulivu, wastahimilivu na wamoja katika kipindi hiki kigumu cha majonzi cha kuondokewa na mpendwa wao rais Mstaafu Mkapa.

Rais huyo mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu amefariki akiwa na miaka 81.

Rais John Pombe Magufuli alitangaza usiku wa kuamkia leo Ijumaa kupitia runinga ya taifa taarifa za kufariki dunia kwa Mzee Mkapa katika hospitali moja jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

''Mzee Benjamin William Mkapa Rais wa awamu ya tatu amefariki. Amefariki kwenye hospitali mjini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa. Niwaombe watanzania tulipokee hili. Taifa limepata msiba mkubwa. Tuendelee kumuombea Mzee wetu Rais Benjamin William Mkapa ambaye ametangulia mbele ya haki," alitangaza rais Magufuli.

Taarifa hiyo hata hivyo haikuweka wazi Rais Mkapa alikuwa akisumbuliwa na maradhi gani.

Katika ukurasa rasmi wa Rais Magufuli wa mtandao wa Twitter rais Magufuli amemuomboleza Mkapa na kusema atamkumbuka "kwa mapenzi yake makubwa kwa Taifa, ucha Mungu, uchapakazi na utendaji wake katika kujenga uchumi."

Rais Mkapa alizaliwa Novemba 1938, Mkoani Mtwara Kusini mwa Tanzania, na aliliongoza taifa hili la Tanzania kwa mihula miwili toka mwaka 1995 mpaka 2005.

Latest News

RAIS TRUMP AKUTANA NA RUNGU LA UDHIBITI KUTOKA FACEBOOK NA TWITTER.
06 Aug 2020 12:53 - Grace Melleor

Mitandao ya kijamii Facebook na Twitter imemuadhibu Rais Donald Trump na kampeni yake kwa kutuma ujumbe ambapo rais huyo [ ... ]

KUMBUKIZI YA SHAMBULIZI LA BOMU LILOWEKA HISTORIA KUBWA DUNIANI.
06 Aug 2020 12:18 - Grace Melleor

Leo Japan inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 75 ya shambulizi la bomu la atomiki katika historia yake.

KESI YA WAKILI SANGA DHIDI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI BADO NI KITENDAWILI.
05 Aug 2020 18:14 - Grace Melleor

Mahakama ya Rufaa ya Tanzania imetupilia mbali uamuzi wa Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.