Star Tv

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John  Myika,  amesema hatagombea ubunge, katika jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam.

Mnyika ambaye amekuwa mbunge wa Kibamba kwa miaka 10 mfululizo, amesema amechukua hatua hiyo ili  apate muda wa kutosha kutumikia nafasi yake ya sasa ya Katibu Mkuu CHADEMA.

 "Haya nilisema kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu 2019, Nyerere aliwahi kuachia Uwaziri Mkuu akabaki kuimarisha TANU, nami sitagombea ubunge 2020, nitumikie ipasavyo Ukatibu Mkuu CHADEMA tushinde chaguzi."-ameandika John Mnyika kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Mnyika alichaguliwa kuwa katibu mkuu wa chama hicho Desemba mwaka 2019 akichukua nafasi ya Dk. Vicent Mashinji ambaye jina lake halikupendekezwa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa chama hicho .

Katika mkutano wa kura za maoni uliyofanyika  jana Jumanne, tarehe 14 Juni 2020, Ernest Mgawe, mwenyekiti wa Chadema katika jimbo la Kibamba, alitangazwa mshindi kwa kupata kupata kura 30, kati ya 71 zilizopigwa.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.