Star Tv

Jumla ya wanachama Milioni 1,023, 911 wa chama cha Mapinduzi, CCM wamejitokeza kumdhamini Mwenyekiti wao Rais Magufuli katika fomu za kuwania kupitishwa na chama hicho kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Hayo yameelezwa leo Jumanne tarehe 30 Juni 2020 makao makuu ya CCM, Dodoma na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally wakati wa hafla fupi ya kuzipokea Fomu za Kugombea Urais wa Tanzania Zilizowasilishwa na Rais Magufuli.

Hafla hiyo fupi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM, Serikali na wanachama wa chama hicho wakiwemo wenyeviti wa chama hicho nzima waliowasilisha kila mmoja fomu za udhamini.

Aidha, Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally Amesema, leo Jumanne saa 10 jioni ndio siku ya mwisho ya uchukuaji na urejeshaji fomu za urais ndani ya chama hicho, na pia amesema, jumla ya wanachama Milioni 1,023, 911 walijitokeza kumdhamini Rais Magufuli kutoka mikoa 32 na jumuiya zake tatu za wazazi, vijana na wanawake

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.